Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akimkabidhi baba wa watoto pacha wanee, Abednego Andrew Mafuluka mkazi wa Kimara Mwisho, Dar es Salaam mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni msaada kwa mapacha hao wanne. Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi cha shilingi milioni 10, kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye. Wa pili kulia ni mama mzazi wa mapacha hao, Sara Dimosso akiwa kabeba watoto wake huku akisaidiwa na nduguye. Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika picha na familia ya Bwana na Bibi Abednego Andrew Mafuluka pamoja na watoto wao mapacha wanne mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya msaada. Bwana Abednego Andrew Mafuluka (katikati) akizungumza kuishukuru Benki ya NMB baada ya kuguswa na kuamua kuwasaidia watoto wao mapacha wanne. Mama mzazi wa watoto mapacha wanne, Sara Dimosso (kulia) pamoja na mume wake, Abednego Andrew Mafuluka akizungumza kuishukuru Benki ya NMB kwa kuwasaidia shilingi milioni 10 iwawezeshe katika malezi ya watoto hao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...