Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza zoezi la makabidhiano ya madawati kutoka Jumuiya ya Mabohora iliyopo hapa nchini, jumuiya hiyo imechangia jumla ya madawati 105 yenye thamani ya shilingi milioni kumi. Hii ni katika kuiunga mkono Serikali kwenye zoezi la kuchangia madawati nchi nzima lililo tangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Madawati hayo yametengenezwa hapa nchini na Kampuni ya Jambo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora, Mhe. Shehe Zainuddin Adamjee naye akizungumza na waandishi wa habari kwenye makabidhiano ya madawati.
Sehemu ya wawakilishi wa Jumuiya hiyo wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Mahiga.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...