Akiwa na siku 85 tangu kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni April 21, 2016, Ally Salum Hapi ameendelea kutekeleza kwa vitendo majukumu aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais John Pombe Magufuli.

Licha ya kusimamia suala la watumishi hewa katika wilaya yake ambao walikuwa 34 na kufikia 101, huku akisimamia vyema na Kulimaliza suala la upatikanaji wa madawati katika wilaya yake ambapo imekuwa changamoto kubwa tangu kutangazwa kwa Elimu bure.

Mkuu wa Wilaya, Ally Salum Hapi ameelendelea na kasi hiyo ya HAPA KAZI TU ambapo leo ametembelea maeneo ya Tandale Hospitali, Uwanja wa Fisi na Soko la Tandale kwa ajili ya kusikiliza kero za wakazi wa maeneo hayo.

Akizungumza na wakazi hao amewataka kuzingatia suala la usafi na kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kuwekea uchafu katika maeneo yao huku akiwasisitiza wale wenye sehemu za kuegeshea magari katika maeneo yao kuyaweka katika mazingira ambayo hayataleta athari.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akiwa na ujumbe wake, wakipita maeneo ya Tandale Uwanja wa Fisi kwa ajili ya kusikiliza kero za wakazi wa maeneo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza na mmoja wa wananchi wakazi wa Maeneo ya Tandale jijini Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...