Uhalifu mtandao bado umeendelea kukua maeneo mbali mbali Duniani – Tishio hili linachukua sura ya kipekee wakati ambapo uhalifu mtandao ume endelea kufanyika kwa ustadi wa hali ya juu huku ukindelea kukua kwa kasi ya kipekee.

Ujuzi mkubwa walionao wahalifu mtandao unatosha kua somo kwa wanaopambana na uhalifu mtandao kujipanga zaidi hasa ukizingatia namna ya ufanyai uhalifu mtandao, umeendelea kubadilika kadri teknolojia inavyobadilika sanjari na inavyokua.

Kuzingatia yote haya moja ya maazimio tuliokubaliana Jijini Johannesburg, Afrika kusini mwaka jana (2015) ni kuhakiki ya kua situ tunakua na watu sahihi wenye ujuzi wa kupambana na uhalifu mtandao bali pia kujenga tabia ya kuwaongezea uwezo na kutengeneza nguvu kazi zetu zitakazo saidia mapambano dhidi ya Uhalifu Mtandao Barani na Duniani kwa ujumla.

Nchi mbalimbali barani zimeendelea kulifanyia kazi hili ikiwa ni pamoja na kupitia upya mitaala yake ili kuhakiki elimu sahihi ya maswala ya usalama mitandao inafundishwa na kuhimiza tabia ya wahusika kuendelea kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara pamoja na kujijengea tabia ya kujifunza kwa kupitia yale yanayo andikwa na wataalam wa usalama mtandao ili kufahamu kinachoendelea katika fani husika kwani Mbinu za kihalifu mtandao zimekua zikibadilika sana kadri teknolojia inavyo badilika pamoja na kukua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...