Watanzania waendelea kuwa na muamko zaidi huku promosheni ikielekea ukingoni.
Wiki iliyopita imekua ni wiki yenye shamrashara nyingi za sikukuu na ikamalizika kwa kufanyika kwa droo ya saba ya promosheni ya ‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ iliyofanyika katika studio za ITV ambapo washindi wengine kumi walitangazwa huku wakiibuka na Tsh Milioni moja kila mmoja.
Droo
hiyo iliyoshuhudiwa na waangalizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
nchini, wakaguzi wa nje na washirika wengine, inafanya idadi ya
washindi kufikia washindi 80 kutoka mikoa tofauti hapa nchini
walioshinda kwenye droo za kila ijumaa ya kila wiki na tayari
wameshapokea pesa zao.
“Tayari tumeshatoa Milioni 80 kwa washindi wetu mpaka sasa lakini pia kuna zawadi kibao ambazo wateja wetu wanajishindia ikiwa ni pamoja na bia za bure, kofia na t-shirts wanazopata baa kila mwisho wa wiki ijumaa na jumamosi tunapoendesha shuguli zetu za mauzo sokoni.

Nawakumbusha
wateja wetu waendelee kushiriki mara nyingi kadiri wawezavyo kwani
kushiriki mara nyingi kunampa nafasi nyingi zaidi za kushinda Mamilioni
ya pesa” alisema Afisa Mipango na Uratibu kutoka Kampuni ya Bia ya
Serengeti - Lulu John Mduma. Pia aliongeza kuwa “siku zote kitu kizuri
hakidumu muda mrefu tunategemea kumpata mshindi wetu wa 100 wiki mbili
zijazo”.
Naye Meneja wa Bia ya Tusker - Jasper Maston Migambile akizungumza na wanahabari mara baada ya droo hiyo alisema, “Droo ya leo imeongeza muamko zaidi kwani kilichonifurahisha zaidi ni kushuhudia mteja mmoja Bwana Gastor Mjakonde kutoka Pwani kushinda mara mbili na kuibuka na Milioni mbili, hii ni bahati ya kipekee lakini inaweza kutokea kwa mtu mwingine kwa droo zinazofuata,”

Mmoja wa washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini, Mr. Geofrey Manangwa kutoka Tanga akifanya maandalizi ya duka lake jipya mara baada ya kupata Milioni moja kutoka Tusker iliyomsaidia kuongezea mtaji wa kufungua duka la nafaka.
HABARI ZAIDI SOMA HAPA
HABARI ZAIDI SOMA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...