Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo, Bomang’ombe. Mahakama ya Tanzania ipo katika maboresho mbalimbali yote yakilenga kuboresha huduma ya utoaji haki, moja ya kipaumbele cha maboresho hayo ni pamoja na kuboresha mindombinu yake kama majengo ya Mahakama, lengo ni kuwa na majengo ya Mahakama za Mwanzo katika kila Kata, Mahakama za Wilaya katika kila wilaya, mikoa na hata Mahakama Kuu.
Mhe. Jaji Mkuu akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Mahakama ya Mwanzo Bomang’ombe baada ya kuizindua rasmi Mahakama hiyo ambayo itakuwa kimbilio la haki kwa wakazi wa eneo hilo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Moshi mara baada ya uzinduzi rasmi ya Mahakama ya Mwanzo Boang’ombe wilayani Hai.
(Picha na Mahakama ya Tanzania).





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...