JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza nyaraka za serikali bandia na kuisababishia serikali kukosa mapato kutokana na nyaraka hizo kutumika.

Watu hao wamekuwa wakitengeneza nyaraka ambazo ni vyeti vya kuzaliwa ,Cheti cha Matokeo ya Kidato cha Nne na Sita, vyeti vya kuhitimu, Kadi za bima mbalimbali pamoja na mihuri mbalimbali ya taasisi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa watu hao wanawahoji juu ya watu walionufaika na vyeti bandia.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hapo pichani) kuhusu Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza nyaraka za serikali bandia na kuisababishia serikali kukosa mapato,leo jijini Dar es Salaam

Kamanda Sirro amesema kuwa watafatilia watu wote wenye vyeti bandia ambao watatajwa na wameajiliwa na serikali katika sehemu mbalimbali.

Aliwataja watu hao kuwa ni Ashrafu Maumba (37) Mkazi wa Buguruni Ghana, Mwamba Seif (38) Mkazi wa Mnyamani pamoja na Mahamudu Zuber (24) Mkazi wa Buguruni.

Nyaraka walizowakuta nazo ni vyeti bandia vya kidato cha nne 50, stika za SUMATRA 20, Vyeti vya Vyuo vya Uuguzi, Vyeti vya Kuzaliwa 10, VETA 10, Cheti cha Darasa la Saba, Siri au Rakili bandia za vyeti vya CBE 10. Leseni za Biashara, nyaraka za bima 100 pamoja na nyaraka za COMESA 100.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akiwaonesha waandishi wa habari nyaraka za serikali bandia,leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka.

Katika upekuzi huo waliweza kukamata mihuri mbalimbali ya Ofisi za Serikali na Binafsi, Muhuri wenye nembo ya bibi na bwana, Karatasi maalum zilizo na nembo za TRA kwa ajili ya kutengeneza kadi za vyombo vya moto Zaidi ya 500, Computa nne, Monitor Screen tatu, printer tatu Generator moja na stabilizer moja.

Baada ya uchunguzi watu hao watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Wakati huo huo jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki aina ya Short Gun Pump Action ikiwa na risasi sita pamoja na pikipiki aina Fekon .

Silaha na pikipiki hiyo walikamata wakati majambazi walikuwa wakitaka kwenda kuvamia na jeshi la polisi lilipata taarifa na kutumia mbinu zao za kuwakamata baada ya kuwakimbiza na kuweza kuacha vitu hivvyo.Na Chalila Kibuda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...