Na John Stephen Dar es Salaam, Tanzania. 

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)-Muhimbili LEO imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa mtoto, Happiness John Josephat ambaye amepandikizwa Pacemaker (betri ya umeme wa moyo) kwenye mfumo wa moyo wake. 
 Mmoja wa madaktari wa moyo walioshiriki kwenye upasuaji huo, Dk Godwin Sharau wa taasisi hiyo amesema upasuaji huo umechukua saa moja na kwamba mtoto anaendelea vuzuri.
 Dk Sharau amesema mtoto huyo amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) ambayo itasaidia kuunganisha mishipa ya fahamu ya umeme wa moyo ambayo inaunganisha vyumba vya moyo vya juu na chini kwenye moyo wa binadamu. 
 “Upasuaji huu ni wa kwanza kufanyika Tanzania. Upasuaji kama huu unafanyika kwa watu wazima, lakini watu wazima hawahitaji upasuaji wa moyo wa kupandikiza. Watoto wanahitaji upasuaji wa moyo wa kuipandikiza. 
 “Tatizo la mtoto huyu ni la kuzaliwa. Na ni nadra kutokea. Inaweza kupita miaka mingi bila watoto kutokea tatizo kama hilo. Upasuaji umefanywa kwa ushirikiano wa madaktari wa moyo na madaktari wa matibabu ya moyo nikiwamo mimi (Dk. Godwin Sharau), Dk Michael Valentine kutoka Marekani, Dk Kisenge na Dk Sulende Kubhoja, Dk wa usingizi, Dk Anjelan Muhozya na madaktari wengine ambao wamesaidia katika upasuaji huu,” amesema Dk Godwin Sharau. 
 Mama wa mtoto huyo, Elitruda Eligi Malley ambaye ni mkazi wa Sakina-Raskazon mkoani Arusha amewashukuru madaktari wa Taasisi hiyo kwa kufanya upasuaji huo na mtoto wake kutoka salama katika chumba cha upasuaji.

Kutoka kushoto ni Dk Michael Valentine kutoka Marekani, Dk Godwin Sharau wa JKCI-Muhimbili, Mama wa mtoto huyo, Elitruda Eligi Malley na Dk Anjelan Muhozya wakifuatilia afya ya mtoto, Happiness John Josephat baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo LEO katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Baadhi ya madaktari wakifuatilia maendeleo ya mtoto, Happiness John Josephat kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo LEO katika taasisi hiyo.
Mama wa mtoto huyo, Elitruda Eligi Malley akimwangalia mtoto wake, Happiness John Josephat baada ya kufanyiwa upasuaji
Baadhi ya madaktari na wataalamu wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya shughuli ya upasuaji kufanyika.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2016

    "PACEMAKER" na siyo peacemaker, in a way you are literally right as the PACEMAKER brings about peace on how the heart is going to function thereafter. Pacemaker in Kiswahili pengine ni "Kisanii mwendo kasi Moyo" KMKM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...