Usiku huu wanachama wa Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) wamemtembelea mwanachama mwenzao Haji Manara ambaye pia ni Afisa Habari wa Simba DC nyumbani kwake Magomeni Kibamba kumjulia hali na pia kushiriki katika maulid maalum aliyoandaliwa na familia yake kumuombea dua kabla hajasafiri kwend nchini India kesho Jumamosi kwa matibabu ya macho ambayo yamekuwa yanamsumbua kwa muda wa wiki moja sasa. Tunashukuru hali yake inazidi kuimarika japo ni jicho moja tu la kulia linaloweza kuona kiasi wakati la kushoto bado halioni. Tunamtakia apate nafuu katika matibabu yake na arudi kuendeleza raha ya kandanda na KFDF akiwa buheri wa afya.
Home
Unlabelled
KFDF YAMJULIA HALI HAJI SUNDAY MANARA Computer
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...