Hapana shaka Bara la Afrika limekua kivutio kwa watu wa kaliba na kadhia zote ulimwenguni wakiwemo viongozi, wafanyabiashara, wawekezaji, watafiti, watalii na wengine wengi
Tukiwa na ugeni wa ziara ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. wiki hii Barani Afrika na wiki ijayo ambapo Rais wa India Pranab Mukherjee, anaanza ziara ya siku sita barani Afrika yenye lengo la kuboresha ushirikiano wa kibiashara, ni vyema tukaendelea kukumbushana machache kati ya mengi kuhusu AFRIKA
1. Bara la Afrika ni la pili kwa ukubwa miongoni mwa mabara saba ya Ulimwengu. Lina kilomita za mraba 30 million, ASIA ndilo bara linaloongoza kwa ukubwa kwani lina kilomita za mraba 44 million.
2. Bara la Afrika ndilo lenye nchi nyingi zaidi duniani likiwa na jumla ya nchi 54 (Sahara Magharibi Ndiyo Nchi Pekee ndani ya AFRIKA ILIYOJITENGA); Bara la Asia ni la pili likiwa na nchi 49
3, Mto Nile Ndio Mto mrefu duniani ambao una urefu wa kilomita 6,650. Pia mto Congo, ambao una urefu wa kilomita 4,700 unashika nafasi ya nane miongoni mwa mito mirefu duniani-mto Nile ndio taswira ya ustaarabu wa mwanadamu duniani (civilization) kwani unaunganisha mataifa 11 YA AFRIKA (Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo-Kinshasa, Kenya, Ethiopia, Eritrea, South Sudan, Sudan na Misri).
4. 30% ya madini yote duniani yanapatikana Afrika huku (asilimia 40 ikiwa ni dhahabu) Nusu ya almasi yote duniani, ikitoka kusini na Afrika ya kati
5. Jangwa la Sahara ndilo jangwa kubwa duniani. likiwa limeenea katika nchi zipatazo 12, Jangwa la Sahara ni kubwa kuliko bara lote la Amerika ya Kaskazini (ikiwemo Marekani Yote).
6. Jiji linaloongoza kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika ni Lagos ambalo liko nchini Nigeria, lina jumla ya watu 21 million (zaidi ya mara nne ya DSM na takirbani nusu ya watanzania wote). Jiji la Cairo lililopo nchini Misri ni la pili likiwa na jumla ya watu 13 million, wakati jiji la Kinshasa linalopatikana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linashika namba tatu kwa kuwa na jumla ya watu 12 millioni, Afrika ni ya pili duniani kwa wingi wa watu ambayo ni sawa na 15% ya watu wote duniani.
7. Kila mmoja ni Mwafrika kwa asili-Vipimo vya kinasaba (DNA) . vimethibitisha kuwa, binadamu wote ulimwenguni wanahusiana na watu wa kale ambao walihama barani Afrika kiasi miaka 125,000 iliyopita. Watu wameanza kuzaliana zaidi katika mabara yote miaka 80,000 baada ya hapo.
8. Bara la Afrika ni bara ambalo linapatikana wanyama wa aina zote yaani wenye kasi zaidi na wanyama wakubwa zaidi. Asilimia 85 ya Tembo wote Duniani wanapatikana Afrika huku ikiwa na asilimia 99 ya Simba wote waliosalia duniani kwa sasa. 25% ya ndege wote duniani wanapatiakana kwenye Bara hili huku Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa likiitaja Hifadhi ya Serengeti Kama eneo pekee la URITHI WA DUNIA kwa sasa (world heritage site) kwani ndiyo pekee iliyosalia kuwa na hayawani na ndege adimu duniani
9. Ziwa Tanganyika lipatikanalo barani Africa, ni ziwa la pili kwa kuwa na kina kirefu ulimwenguni. Ziwa hili limekwenda chini kwa urefu wa zaidi ya kilomita 1.7. Hii ni pungufu ya mita 200 nyuma ya ziwa linaloongoza kwa kina kirefu ambalo linapatikana nchini Russia.
10. Ziwa Victoria ni ziwa la pili kwa ukubwa ulimwenguni. Pia ni chanzo cha mto Nile. Kadhalika Ziwa Nyasa/Malawi linalozigawa Tanzania na Malawi ndilo lenye aina nyingi/species za samaki wa maji baridi kuliko ziwa lolote duniani
11. Nchi zote za Afrika kasoro Ethiopia na Liberia zimepita katika Kongwa la Ukoloni kwa miongo kadhaa huku Ghana ikiwa ya kwanza ilihali Zimbabwe ikiwa ya mwisho kujinasua kutoka kwenye kongwa la mkoloni
12. Tafiti zinaonesha kwamba 40% ya watu wazima hapa Afrika wako kwenye lindi la UJINGA wa kwa maana ya kutojua kusoma wala kuandika (Illiteracy) huku theluthi mbili kati yako wakiwa ni wanawake
HATA HIVYO RIPOTI YA BENKI YA DUNIA YA MWAKA 2013 INAIWEKA AFRIKA KAMA BARA MASIKINI ZAIDI KULIKO MABARA YOTE ULIMWENGUNI (AFRIKA NZIMA INACHANGIA 2.4% TU YA UTAJIRI/PATO LOTE DUNIANI/GDP)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...