Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakitazama gari Kaparata kwenye banda la Shirika la Viwanda Vidogo vidogo SIDO kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Gari hilo limebuniwa na kutengenezwa na Mtanzania Jacob Luis, wa Kaparata Engineering.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, ametembelea banda la Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, 2016 yanayoendelea pale viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mayingu alitembelea banda hilo ili kujionea na kupata maelezo ya kina jinsi shirika hilo linavyoendeleza viwanda vidogovidogo ambavyo vinahitajika sana kwa sasa ukizingatia mkakati mkubwa wa serikali ya awamu ya Tano ambayo iemdhamiria kuifanya bTanzania kwua nchi ya viwanda na hivyo kupanua wigo wa ajira kwa Watanzania.

Mkurugenzi Mkuu huyo amabye alifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, alipokelewa na Msimamizi Mkuu wa banda hilo, Kalumuna Benedicto, na alitembezwa maeneo mbalimbali na kujionea mashine mbalimbali zilizobuniwa na kutengenezwa na watanzania.

Mbunifu wa gari hilo, Jacob Luis, akihojiwa na mwandishi wa habari kuhusu ubunifu huo


Pia alipata fursa ya kujionea gari lililobuniwa na kutengenezwa na Mtanzania Jacob Luis, wa Kaparata Engineering. Gari hilo lina injini yenye ukubwa wa CC 900 na linatumia mafuta ya petrol, likitumia lita moja ya petrol kwa kilomita 15 na linabeba watu watano na mzigo wa kilo 500.

Kwa mujibu wa maelezo ya mbunifu Jacob Luis, gari hilo ni maalum kwa shughuli za shamba, kubeba maharusi, shughuli za kijeshi, polisi na zile za kiulinzi.

Mkurugenzi huyo pia alitembelea mabanda washirika wa PSPF, likiwemo lile linalokusanya wajasiriamali wanawake kutoka nchi nzima ikiwemo Zanzibar, hali kadhalika Mkurugenzi Mkuu huyo alitembelea Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF, LAPF, GEPF NA PPF.

 Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakati akikagua mashine zilizokuwa zikionyeshwa kwenye banda hilo la SIDO
 Muangalizi Mkuu wa banda la SIDO, Kalumuna Benedicto, (kushoto), akimpatia maelezo, Mkurugenzi Mkuu Mayingu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi kuhusu mashine hizi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...