Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akiangalia jinsi askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wanapokuwa wanazima moto katika matukio mbalimbali. Kulia ni Kaimu Kamishna wa Jeshi hilo Mkoa wa Mwanza, ACF Hamidu Nguya. Masauni alifanya ziara katika Ofisi za Jeshi hilo jijini Mwanza kwa lengo la kujua jinsi gani jeshi hilo linavyofanyakazi mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwasalimia Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Mwanza wakati alipokuwa anawasili katika ofisi za Jeshi hilo, jijini Mwanza. Masauni aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti), Kaimu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, ACF Hamidu Nguya (wanne kulia) na akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo mkoani humo. Masauni alifanya ziara katika ofisi za Jeshi hilo kwa lengo la kujua jinsi gani jeshi hilo linavyofanyakazi katika matukio mbalimbali jijini Mwanza. Hata hivyo, Masauni aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...