Mashindano ya mbio za baiskeli kanda ya Ziwa yaliyondaliwa na Chama cha Mbio za baiskeli Tanzania (CHABATA) yanayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia inayomiliki migodi ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara yanatarajiwa kutimua vumbi Julai 16,2016 mkoani Shinyanga. 

Mashindano hayo ya kusaka bingwa wa mbio za baiskeli kwa upande wa wanaume na wanawake kanda ya ziwa yanajumuisha washiriki 120 kutoka mikoa sita ya kanda ya ziwa ambapo kila mkoa utatoa washiriki 20. 

Akizungumza leo wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa uongozi wa CHABATA kwa ajili ya mashindano hayo,Makamu wa rais wa Kampuni ya Acacia Deo Mwanyika alisema mashindano hayo yatakuwa katika makundi matatu,ambapo kundi la kwanza ni la wanaume, pili wanawake na kundi la tatu ni wafanyakazi wa migodi ya Acacia ambao nao watashiriki katika kundi lao. 
 Makamu wa Rais wa Kampuni ya Uchimbaji dhahabu ya Acacia, Deo Mwanyika akikabidhi jezi kwa rais wa Chama Mbio za Baiskeli Tanzania (CHABATA), Godfrey Jax Mhagama kwa ajili ya mashindano ya mbio za baiskeli Kanda ya Ziwa Victoria yatakayofanyika siku ya Jumamosi, Julai 16,2016. 

Alisema ni mwaka wa tatu sasa Acacia imekuwa ikishirikiana na CHABATA kuendesha mashindano ya mbio za baiskeli kanda ya ziwa yenye mikoa sita ambayo ni Shinyanga,Mwanza,Geita,Simiyu,Mara na Kagera. 

“Kampuni ya Acacia inajali wananchi katika maeneo mbalimbali,na kwenye eneo hili la michezo ufadhili wetu umekuwa mkubwa ambapo kila mwaka huwa tunatoa kiasi cha shilingi milioni 130 kusaidia kuendesha mashindano haya…tunafurahi kuwa mashindano haya kila mwaka yamekuwa ni mazuri na yanapendwa sana na wananchi wa kanda ya ziwa”,alieleza Mwanyika.
 “Tangu tulivyoanza mwaka 2013 tumekuwa tukijitahidi kuboresha mashindano haya,tumekuwa tukitoa zawadi nyingi na nzuri lengo kubwa ni kuinua vipaji kwenye maeneo yanayotuzunguka ndiyo maana tumewapa kipaumbele wakazi wa maeneo haya”,aliongeza. Mwanyika alisema kilele cha mashindano hayo kimekuwa kikifanyika Kahama kwa sababu kuna migodi miwili na kwamba hata mwaka huu yatafanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...