Waziri wa Habari Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya TAYI Tanzania Ndh Abdalla Othman Miraji wakati akihudhuria fainali za Kombe la Masauni and Jazeera lililofanyika jana usiku katika viwanja vya Mnazi Mmoja kati ya Kilimani na Kisimamanjongoo, kabla ya mchezo huo kulikuwa na mchezo wa utangulizi kati ya Maveterani wa Kikwajuni na Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, katika mchezo huo timu ya Baraza imeshinda bao 1--0.
Timu za Baraza na Maveterani zikiingia uwanjani tayari kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika wakati wa fainali hiyo Timu ya Maveterani wa Kikwajuni wakiongozwa na Mhe. Mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng Hamad Yussuf Masauni kulia na Timu ya Baraza ikiongozwa na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salum Jazeera.
Wachezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni wakimsikiliza Waziri wa Michezo Mhe Nape Mnauye akitowa nasaha zake kwa Wanamichezo waliohudhuria fainali hiyo na kuupongeza Uongozi wa Kamati ya Mashindano hayo Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
Wachezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni wakimsikiliza Waziri wa Michezo Mhe Nape Mnauye akitowa nasaha zake kwa Wanamichezo waliohudhuria fainali hiyo na kuupongeza Uongozi wa Kamati ya Mashindano hayo Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akimiliki mpira akijiandaa kumpita mchezaji wa Timu ya Baraza la Wawakilishi wakati wa mchezo wao wa kirafiki. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...