Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Zelothe Stephen amewaapisha wakuu wa wilaya mbalimbali za mkoani humo mapema hii leo (5/ 07/ 2016)

akitoa nasaha zake kwa wakuu wa wilaya hao ambao ni Mh.Said Mohammed Mtanda (Nkasi), Dkt. Halfan Boniface Haule (Sumbawanga) pamoja na Mh. Julieth Nkembanyi Binyura (Kalambo) mkuu huyo wa mkoa amewataka kusimamia changamoto kadha wa kadha huku akipigia msumari suala la uwazi na uwajibikaji na kubainisha changamoto kubwa ya mkoa wa rukwa ni kuongezeka kwa kasi kwa uharibifu wa mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh.Said Mohammed Mtanda akila kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Zelothe Stephen.
Wakuu wa Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Rukwa, Kutoka kushoto Mh.Halfani Boniface Haule (Sumbawanga) Mh.Said Mtanda (Nkasi) akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Bi.Julieth Binyura Nkembanyi Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh.Said Mtanda mara baada ya kuapishwa moja kwa moja ameanza kazi kwa kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambapo alisisitiza umuhimu wa watumishi mbalimbali waliomo wilayani Nkasi kujtuma na kufanya kazi kwa bidii aidha alitilia mkazo suala la watumishi kutenda haki na kuwahudumia wananchi kwa wakati
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh.Said Mtanda akipokea taarifa ya Wilaya toka kwa Katibu Tawala wa Wilaya Ndg Chonya (Alyesimama)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...