Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah leo ametembelea zahanati ya Kilolo mapema asubuhi kwa lengo la kujionea mazingira ya zahanati hiyo.
 Akiwa hapo alikutana na Daktari mfawidhi Dkt.  Selemani Jumbe ambapo pamoja na mambo mengine alimwambia kuwa  wanatamani sana kuwa na vifaa vya kufanyia kazi kama vile Full Blood Picture Machine, Ultra Sound, Na X-ray ambavyo anasema kwa wilaya nzima hakuna huduma ya X-ray hivyo inawawia vigumu kukamilisha tiba kwa wagonjwa wenye kuhitaji huduma hiyo.
 DC Asia pia alikutana na wazee wa mji wa Kilolo ambao  wameiomba serikali kuwapatia watalaamu pamoja na vifaa vya upasuaji kwa kuwa tayari walishapata jengo la upasuaji kutoka kwa mdau wa maendeleo ila  wanakwama kuanza kutumia huduma hiyo ya upasuaje kufuatia ukosefu huo wa wataalamu na Vifaa. 
Mhe Mkuu wa Wilaya huyo aliwaahidi kufuatilia na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo, huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza miundombinu iliyopo wilayani humo kwa faida yao
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah leo ametembelea zahanati ya Kilolo mapema asubuhi kwa lengo la kujionea mazingira ya zahanati hiyo. Akiwa hapo alikutana na Daktari mfawidhi Dkt.  Selemani Jumbe
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah akiwa na Dkt. Selemani Jumbe mwenye koti jeusi na Bw. Ephron msuva mtaalamu wa maabara. alipotembelea zahanati ya Kilolo mapema asubuhi kwa lengo la kujionea mazingira ya zahanati hiyo. Akiwa hapo alikutana na Daktari mfawidhi Dkt.  Selemani Jumbe
  
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah akipata maelezo ya jinsi vipimo mbalimbali vinavyopimwa katika maabara ya zahanati ya Kilolo alipotembelea mapema asubuhi kwa lengo la kujionea mazingira ya zahanati hiyo. 
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...