Aliekuwa Mpinzani wa karibu wa Bi.Hillary Clinton katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kupewa ridhaa ya kubombea Urais wa Marekan kupitia Chama Cha Democrats, Bernie Sanders, amemuidhinisha Mwanamama huyo ambaye pia ni mke wa Rais wa zamani wa Marekani,(Billy Clinton), kupeperusha bendera ya Chama chao kwenye kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa taifa hilo lenye nguvu duniani unaotazamiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Bernie Sanders amemuidhinisha Bi.Hillary Clinton wakati wa mkutano wa pamoja wa kampeni uliofanyikia Portsmouth, New Hampshire.

Kwa kumuidhinisha huko Bi. Hillary Clinton, Sanders amesema kuwa amezika moja kwa moja fununu na tetesi zilizokuwa zinaenea kwamba hatomuidhinisha Clinton na huenda akachagua kuwa mgombea binafsi. Habari hizi pia ni pigo kwa mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump ambaye alikuwa na matumaini ya kuwapata wapenzi wa Bernie Sanders kwa njia moja au nyingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...