Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kusherekea sikukuu ya Eid El Fitri, Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ndiyo wasambazaji wa ving'amuzi vya DSTV nchini imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima ambao wanaishi katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, misaada ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kusaidia kubadilisha maisha ya watoto hao.

Misaada ambayo imetolewa kwa watoto hao ni Cherehani 4, kapeti 12, vikombe 60, sahani 40, magodoro 11, shuka 40, tenga za nguo 3, jagi 6, beseni kubwa 3, sufuria 9, chupa za chai 4 na mikeka 6.Akizungumzia misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo Multichoice imekuwa ikitoa kwa kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia kuishi maisha bora lakini pia kuwapatia msaada ambao unaweza kuwasaidia kuwa na uwezo wa kuingiza kipato.

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa kituo cha Al--Madina.

"Multichoice tumekuwa tukitoa misaada yetu kwa kituo hiki tangu 2009 na leo tumewaletea mwingine ikiwa ni kila mwaka tunafanya hivyi lakini kwa mwaka huu tumeleta pia Cherehani ambazo zitawasaidia kupata kipato,
"Pamoja na hayo pia tumewafungia king'amuzi ambacho watoto watakuwa wakiangalia vipindi balimbali baada ya kurejea nyumbani na tuna chaneli mbalimbali za vipindi vya watoto na burudani kwahiyo tunaamini kuwa watoto watafurahi," alisema Chande.

Nae mlezi wa kituo hicho, Bi. Kuruthum Yusuf aliwataja Multichoice kama kampuni ambayo imekuwa mstari wa mbele kuwapatia misaada na kuyaomba makampuni mengine kuwa na utaratibu kama wa Multichoice wa kuwasaidia misaada kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao wanahitaji misaada ili kuboresha maisha yao.

Mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Al-Madina akizungumza kuhusu msaada ambao wamepokea na jinsi ambavyo Multichoice Tanzania imekuwa ikiwapatia misaada. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande.

"Tangu walipotufahamu wamekuwa wakitupatia misaada kila mwaka, niwashukuru sana kwa moyo wao na kutoa sio utajiri ila tu wana moyo wa kutoa na hata wenngine wanatakiwa kuwa na moyo kama wao (Multichoice) wa kusaidia," alisema Bi. Kuruthum.Pamoja na hayo pia, Bi. Kuruthum alieleza kuwa kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto ya vifaa vya shuleni kwa watoto ambao wanasoma.

Kutokana na msaada ambao umetolewa na Multichoice kwa watoto wa kituo cha Al-Madina ambacho kina watoto 57, wasichana wakiwa ni 23 na wavulana ni 34 basi ni wazi kuwa kama wakitumia msaada huo vyema basi kwa namna moja au nyingine wanaweza kubadilisha maisha yao kwa hatua fulani ambayo awali hawakuwa nayo kama vile kutumia cherehani kwa kushona nguo na kujiongezea kipato.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Sumalu akitoa neno la ufunguzi kuhusu misaada ambayo imekuwa ikitolewa na Multichoice Tanzania pamoja na historia fupi ya kituo hicho.


PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...