Na Abel Daud wa Globu ya Jamii Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jeneral Mstaafu Emanuel Maganga,amewaagiza wakuu wapya wa Wilaya mkoani humo kwenda kusimamia miradi mbalimbali ya huduma za jamii na kutatua kero zao zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.
Ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya sita walioteuliwa na Rais John Magufuli,ambapo Mkuu huyo wa Mkoa amewataka Wakuu hao wa Wilaya kutoa kipaumbele katika kutenga maeneo kwa ajili ya wananchi watakaondolewa katika maeneo ya hifadhi hasa wafugaji.
Masuala mengine ambayo Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza Wakuu wa Wilaya ,ni kusimamia kero za mda mrefu zinazo wakabili wananchi hao kama maji,usambazaji wa pembejeo pamoja na rushwa.
Aidha Brigedia Jeneral Maganga amewaagiza Wakuu hao wa Wilaya kusimamia utunzaji wa mazingira huku akitumia nafasi hiyo kuutaka umoja wa Mataifa kupitia shirika la kuhudumia wakimbizi,UNHCR kuangalia matumizi ya gesi asili ili kulinda mazingira ya Mkoa wa Kigoma ambayo yanaharibiwa na wakimbizi wanaokata miti kwa ajili ya matumizi ya kuni.
Wakiongea mara baada ya kula kiapo,Wakuu wapya wa Wilaya wameahidi kuendeleza yote yaliyoanzishwa na Rais John Magufuli ambayo ni kuwapigania wananchi wanyonge na maskini na kuhakikisha maendeleo tarajiwa yanapatikana.
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mhe Luis Peter Bura aipokea nyenzo za kazi toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jeneral Mstaafu Emanuel Maganga
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Renard Anga akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jeneral Mstaafu Emanuel Maganga
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Elisha Marco Gagist akipokea nyenzo za kazi toka kwa Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jeneral mstaafu Emmanuel Maganga
Mkuu wa wilaya ya Uvinza Bi.Mwanamvua Mlindoko akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jeneral mstaafu Emmanuel Maganga
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Elias Mkisi akila kiapo







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...