Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa amemteua Bw. Masanja Kungu
Kadogosa(pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni ya Reli
Tanzania(TRL). Uteuzi huo umeanza Julai 01, 2016.
Bw. Kadogosa, mwenye umri wa miaka 41, mapema Februari 4, 2016 aliteuliwa na Serikali
kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL baada ya Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa awali Mhandisi Elias Mshana kuanza likizo ya kustaafu.
Aidha kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa juu katika TRL Bw. Kadogosa alikuwa Mkurugenzi wa Mikopo katika Benki ya ya Maendeleo ya TIB.
Kitaaluma Mkurugenzi huyo
mpya ni msomi wa Masuala ya Uhasibu, Usimamizi wa Fedha na Benki akiwa na
Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara aliofuzu katika Chuo kikuu cha Umea mwaka 2004
nchini Sweden.
Imetolewa
na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Ofisi
ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Dar es
Salaam,
Julai
15, 2016



Real good. Keep it up Masanja
ReplyDelete