Na John Nditi, Morogoro
POLISI mkoani Morogoro inamshikilia Kijana Deodatus Simba (26) mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kupatikana akiwa amevaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kinyume na sheria akiwa si askari wa Jeshi hilo.
Kamada wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema leo ( Julai 15) mjini Morogoro ya kwamba Julai 13, mwaka huu majira ya saa 10 jioni maeneo ya standi ya Msamvu , Manispaa ya Morogoro,
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa katika harakati za kutafuta usafiri wa kuelekea mkoani Dodoma .
Alisema ,baada ya kukamatwa na kuhojiwa uchunguzi wa awali umeonesha kuwa mtu huyo hakuwa askari wa JWTZ , hivyo atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Aidha , alipohojiwa na waandishi wa habari ofisini kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa kuhusu kazi yake halisi , alidai kuwa yenye ni mfanyabiashara wa kuunza nguo za mitumba .
Deodatus Simba (26) mkazi wa Dar es Salaam, ambaye ni mfanyabiashara wa mitumba aliyekamatwa Julai 13 mwaka huu eneo la stendi ya Msamvu , katika Manispaa ya Morogoro akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati akiwa katika harakati za kutafuta usafiri wa kuelekea mkoani Dodoma
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei ( kulia) akimuonesha kwa wanahabari Deodatus Simba (26) mkazi wa Dar es Salaam, ambaye ni mfanyabiashara wa mitumba aliyekamatwa Julai 13 mwaka huu eneo la stendi ya Msamvu , katika Manispaa ya Morogoro akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati akiwa katika harakati za kutafuta usafiri wa kuelekea mkoani Dodoma
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei ( kulia),akiwaelezea waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusu mtuhumiwa Deodatus Simba (26) mkazi wa Dar es Salaam, ambaye ni mfanyabiashara wa mitumba aliyekamatwa Julai 13 mwaka huu eneo la stendi ya Msamvu , katika Manispaa ya Morogoro akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati akiwa katika harakati za kutafuta usafiri wa kuelekea mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei ,julai 15, mwaka huu akionesha kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) moja ya kiroba ilichohifadhiwa dawa zinazodhaniwa ni za kulevya aina ya Heroine kete 16 na vitu vingine kutoka kwa watuhumiwa wanne waliokamatwa Julai 14, mwaka huu eneo la Chamwino, Manispaa ya Morogoro.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...