Jeshi la Polisi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam limemnasa raia wa Nigeria, aliyetambulika kwa jina la Dede Eke (45) baada ya kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroine kilo tano uwanjani hapo.
Akizungumza na Uwazi, ofisini kwake Ijumaa iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Martin Otieno (pichani) alithibitisha kukamatwa kwa Mnigeria huyo siku hiyo akasema kulitokana na kuimarisha ulinzi uwanjani hapo na kufungwa mashine za kisasa za uchunguzi.
“Ni kweli tumemkamata Mnigeria Bede Eke katika Uwanja wa Ndege Dar na kilo tano za dawa za kulevya aina ya heroine wakati akitaka kuondoka kwenda Lagos, Nigeria kwa ndege. Dawa hizo zimepelekwa kwa mkemia mkuu kwa uchunguzi na kujua thamani yake.
“Dede alikuwa ameficha madawa hayo katika begi dogo jeusi ambalo alishonea madawa ndani kisha akalitumbukiza ndani ya begi kubwa, amenishangaza, alidhani hatupo makini!” alisema kamanda huyo na kuongeza kuwa polisi wanamhoji mtuhumiwa huyo kujua alikozipata na upelelezi ukikamilika tutamfikisha mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2016

    The mdudu, yale yale upelelezi wa nini tena? Rais wetu Magufuli alishasema mtu akishakutwa na Madawa hakuna tena mambo ya upelelezi mfungeni haraka sana hao watu ni washenzi funga kabisa ili iwe fundisho kwa washenzi kama hao

    ReplyDelete
  2. Kwa nini huwa tunafichwa sura zao?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2016

    gloves ziko wapi? tuwe proffessional

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...