Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SASA kuiona Yanga vs Medeama kiingilio ni shilingi elfu 5 Kwa viti vya kijani na bluu, Kwa viti vya machungwa ni 10,000, VIP B&C ni 20,000 na VIP A ni 30,000.
Huo unakuwa ni mchezo wa tatu kwa Yanga ikiwa katika mechi za mbili za awali wamepoteza dhidi ya Mo Bejaia na TP Mazembe uliochezwa katika uwanja wa Taifa na kwenye mchezo huo Klabu ya Yanga iliwapa fursa mashabiki wa mpira kuingia bure kushuhudia mtanange huo.
Uongozi wa Yanga umeomba wanachama wake kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia mchezo huo ambapo kwa sasa kikosi kipo tayari kwa ajili ya ushindi na hawatataka kupoteza tena.
Waamuzi wa mchezo wa Yanga na Medeama wanatarajiwa kutoka nchini Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din ambaye ni mwamuzi wa kati, akisaidiwa na Ayman Degaishi, Samir Gamil Saad na wa akiba akiwa Mohamed Maarouf Eid Mansour.
Kamishna wa mechi ni Pasipononga kutoka nchini Zambia huku msimamizi wa waamuzi akiwa Mfubusa Bernard wa Burundi na msimamizi wa mchezo huo ni kutoka nchini Afrika Kusini Ian Peter Keith Mc Leod.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...