Kuelekea Mtanage wa kukata na Shoka kati ya  Yanga dhidi ya Medeama ya Ghana ikiwa ni mchezo wa tatu wa kombe la shirikisho hatua ya makundi kikosi cha Yanga  chini ya Mholanzi Hans Van De Pluijm  akisaidiwa na Juma Mwambusi wamendelea kujifua Katika viwanja vya Boko jijini Dar es Salaam leo.

Yanga wamepoteza michezo yake miwili ya mwanzo na katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mo bejaia ya nchini Algeria walipoteza kwa goli 1-0 wakiwa ugenini na mechi ya pili ni kwenye dimba la taifa dhidi ya TP mazembe. 

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi Amisi Tambwe ameanza mazoezi binafis na kesho anatarajiwa kujumuka na wenzake baada ya maendeleo yake kuendelea vizuri.
Kikosi cha Timu ya Yanga wakijifua kwaajili ya kuingia  dimbani Julai 16 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...