Mbunge wa Jimbo la Ilala Mh. Mussa Zungu (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yenye thamani ya Sh. Milioni 27, sambamba na kukabidhiwa madawati 30 kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa karume, Haji Bechina (kulia) yenye thamani ya milioni 36, hafla hiyo ilifanyika Mtaa wa Karume, Jijini Dar es Salaam. wakwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Ilala Saady Khimji .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es SalaamMh. Paul Makonda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa hafla ya kukabidhiwa mfano wa hundi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu yenye dhamani ya Sh. Milioni 27 kwa niaba ya uchangianji wa madawati kwa kuitikia wito wa Rais Magufuli na katika hafla hiyo mwenyekiti wa Mtaa wa Karume, Haji Bechina na yeye alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam madawati 30 yenye dhamani ya Sh. Milioni 36.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume, Haji Bechina akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda mara baada ya hafla ya kukabidhiwa hundi ya milioni 27 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mh. Mussa Zungu na kupokea madawati 30 yenye dhamani ya Milioni 36 kutoka kwa Mwenykiti huyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...