TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam jana Jumamosi imefanya upasuaji mkubwa na kuweka betri katika moyo wa mtu wa makamo kwa mafanikio.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Profesa Mohamed Janabi ameiambia Globu ya Jamii jioni hii kwamba ana furaha kwa kufanikiwa kwa upasuaji huo ambao amesema umefanyika mara ya kwanza kufanyiwa mtu wa makamo nchini Tanzania.
“Tumeweka kifaa hicho ambacho kitaalamu kinajulikana kama Pacemaker CRTD kwa mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 68 ambaye moyo wake umechoka na hivyo kushindwa kusukuma damu kwenda kwenye mishipa ili isafiri mwilini na yeye aweze kuishi,” alisema Profesa Janabi.
"Hii ni hatua muhimu kwa taasisi hii kwani mafanikio haya yanatupa hamasa ya kuongeza juhudi za kuokoa maisha ya Watanzania wengi hapa hapa nyumbani", alisema Profesa Janabi
Ameongezea kuwa hivi karibuni JKCI ilifanikiwa kufanya upasuaji mwingine wa kwanza na kuweka betri katika moyo wa mtoto mwenye umri wa miaka sita.
Alisema utendaji kazi wa moyo wa mgonjwa huyo ulikuwa chini ya kiwango cha asilimia 20 ndio maana mgonjwa huyo amefanyiwa upasuaji huo ili betri hiyo iweze kumsaidia moyo wake kufanya kazi sawa sawa.
Dkt Kisenge amesema JKCI imefanya upausaji huo kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchini Kenya.
Ni hatua nzuri ya kuboresha zaidi huduma za moyoni, endeleza kazi nzuri.
ReplyDelete