TIMU
ya Yanga yenye makao yake Mtaa wa Twiga na Jangwani imefanikiwa
kupata ushindi wake wa kwanza katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho,
baada ya kupata goli 1-0 lililofungwa na Mchezaji wa kimataifa kutoka
nchini Burundi, Amisi Tambwe dakika ya tatu ya mchezo dhidi ya Timu ya
Mo Bejaia ya nchini Algeria, mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa,
Jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya kupata ushindi huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans
Van De Pluijm amesema ushindi huu umempa nguvu katika kuelekea mchezo
unaofuata dhidi ya TP Mazembe.
Pluijm amesema kuwa, wachezaji wake wamecheza vizuri sana
na wameweza kulinda goli katika dakika zote ingawa kuna makosa madogo
madogo yaliyojitokeza ila anawapa hongera kwa jitihada walizozifanya.
Naye
Nahondha wa Yanga, Vicent Bossou amesema wamefanya kazi kubwa sana
katika kuhakikisha wanatoka ushindi na wamecheza timu nzuri sana yenye
uzoefu wa muda mrefu wa michuano ya kimataifa ila anawapongeza pia
wachezaji wenzake kwa jitihada walizozifanya.
Baada ya ushindi huo Yanga wanaendea kusalia katika
nafasi ya nne wakiwa na alama nne huku mchezo kati ya Mazembe na Medeama
ukitarajiw kuchezwa kesho nchini Ghana.
Mshambuliaji wa Yanga, Obren Chirwa akiwa katikati ya Mabeki wa Timu ya Mo Bejaia.
Washabiki
wa Timu ya Yanga wakiishangilia timu yao baada ya kupata ushingi dhidi
ya Timu ya Mo Bejaia ya Algeria, katika Mechi ya Kombe la Shirikisho
iliyopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga
imeshinda Bao 1-0.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...