Viongozi wa serikali, Vyama vya siasa na wabunge wakisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam kwa ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ya Bombardier, Novemba 13, 2016. Wote walikwenda Urambo Tabora kumzika Spika Mstafu Samuel Sitta Novemba 12, 2016. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mama Mary Majaliwa , Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Home
Unlabelled
SAFARI YA KUTOKA TABORA, DODOMA HADI DAR KWA BOMBADIER Q400 YA ATCL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nani alilipa nauli? Serikali au watu binafsi?
ReplyDeleteMdau wa mwanzo hapo juu, binafsi nadhani waheshimiwa hao, watakuwa wametekeleza kwa vitendo ile kauli ya Mh. Rais siku ile ya uzinduzi rasmi wa ndege hizo mpya, khususa alipoongelea suala zima la gharama za usafiri aliposisitiza hakuna kuangalia hadhi wala cheo cha mtu, unless otherwise..
ReplyDeleteMNAONA HIYO PICHA ILIVYO PENDEZA? WOTE MKO KWENYE NDEGE MOJA, HIYO NDIYO SAWA, NA NINAWAOMBA SANA JARIBUNI KUACHA TOFAUTI ZENU ILI NCHI IWE NA UMOJA NA MSHIKAMANO KAMA MLIVYO KATIKA NDEGE HIYO PLEASE.
ReplyDeleteDR, JAMESSY
Nimeipenda hiyo sitting plan ya Mbowe na Dr Tulia na wanazungumza pamoja ,hakuna kuonyesha utofauti wa mjengoni,safi sana wakuu
ReplyDelete