Bondia Vijender Singh leo amefanikiwa kulinda ubingwa wake wa WBO Asia Pacific Super-Middleweight kwa kumtoa Francis Cheka wa Tanzania kwa TKO raundi ya tatu katika uwanja wa Thyagaraj Stadium jijini New Delhi, India.
Vijender, aliyenyakua medali ya shaba katika michezo ya Olympiki mwaka 2008 huko Beijing, China, hajawahi kupoteza mchezo katika michezo minane aliyocheza.
Kwa mujibu wa tipota wa Globu ya Jamii huko New Delhi, mpambano huo uliovutia mamia ya mashabiki, refarii ilibidi asimamishe mpambano katika raundi ya 3 baada ya Cheka kuzidiwa.
Francis Cheka na mpinzani wake Vijender Singh wa India wakijinadi kabla ya pambano lao
Aibu....India dah......hata ktk ramani haipo......
ReplyDeleteWaandishi wa habari tunavyotoa habari ni muhimu kuwa na taarif kamili. Hii game ya cheka na Singh sidhani kama Cheka alizidiwa ila kwa uelewa wangu mdogo nadhani kunatatizo lilimpata Cheka wakati wa pambano na ndio maana waliamua kumaliza mchezo. Sio fahari kuandika habari kwa ushabiki bila kuzingatia ukweli. Ni vyema jamii ikaelewa ukweli ili wadau wa michezo hususani mchezo wa ngumi wakajua kipi cha kufanya badala ya kuandika habari bia kuzingatia ukweli halisi.
ReplyDelete