Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Simon Msanjila, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST)  Profesa Mark Mwandosya na mwenyeketi wa baraza la chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Profesa Penina Mlama kwa pamoja wakiwa katika maandamano kuelekea katika ukumbi wa Nyerere kabla ya hafla kuanza.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Simon Msanjila akihutubia katika hafla hiyo ya mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Mbeya University of Science and Technology - MUST) kilichopo mkoani mbeya, Mh.Msanjila amekipongeza chuo hicho kwa kuongeza baadhi ya mafunzo ikiwemo mafunzo ya ufindi na mafunzo ya sayansi ya kiafya kwa kushirikiana na hospitali ya Rufaa mkoani mbeya.Pia mh.Simon Msanjila ametoa wito kwa kila mtu mwenye uwezo wa kujifunsa mafunzo ya sayansi na teknolojia yatolewayo katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia kilichopo mkoani mbeya na kuwataka wahitimu kuzikimbilia fursa mbalimbali  haswa katika harakati za kutafuta ajira. Sehemu  ya wahitimu wa stashahada ya kawaida na stashahada ya kwanza katika fani mbalimbali za sayansi na teknolojia wakitunukiwa. Jumla ya wahitiumu wote waliomaliza kozi mbalimbali ni 804 ambapo idadi kubwa ni jinsia ya kime.Wahitimu sambamba na wageni waalikwa na wafanyakazi wa chuo hicho cha sayansi na teknolojia walio hudhuria hafla hiyo ya mahafali ya nne ya MUST yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyerere uliopo chuoni hapo mkoani Mbeya.PICHA NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...