MAONYESHO makubwa ya vyuo vya nje yanatarajiwa kuanza leo tarehe 21 Desemba na kumalizika kesho Desemba 22 mwaka huu katika uwanja wa Makumbusho ya Azimio la Arusha, Jijini Arusha.Kwa mujibu wa Meneja wa Global Education Link (GEL) tawi la Arusha, Regina P. Lema uwanja huo ambao maonyesho yatafanyika unatazamana na Mnara wa Mwenge.

“GEL ndio tunaoendesha maonyesho haya kwa kushirikiana na vyuo vya nje ambavyo baadhi yao tayari vimeshatuma wawakilisha wao. Maana yake ni kwamba watu watapata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa GEL au hao wawakilishi waliotoka nje ili kupata ufahamu mpana zaidi kuhusiana na suala la kusoma nje,” alisema.

Regina alifafanua kuwa baadhi ya vyuo ambavyo vimetuma wawakilishi watakaoshiriki maonyesho hayo ni Lovely Professional University, Sharda University, Chandigarh University na Maharishi Markandeshwar University vyote vya nchini India.

“Nawakaribisha watu wa Arusha na vitongoji vyake kuja kujionea masuala ya namna ya kusoma nje ya nchi, pamoja na uchaguzi wa kozi za kusoma,” aliongeza Mkurugenzi Mkuu wa GEL, Abdulmalik Mollel na kufafanua kuwa lengo la maonyesho hayo ni kufahamishana kozi mbalimbali zinazotolewa nje ya nchi.

“Kuna kozi za kila aina zikiwamo za injinia katika masuala mengi tofauti yakiwamo ya petroli na gesi. Pia kozi za biashara, masoko, afya, udaktari, madini, uchumi na nyingine nyingi,” aliongeza na kufafanua kuwa vyuo ambavyo mtu anaweza kupatiwa maelezo katika maonyesho hayo ni vya nchi nyingi tofauti duniani vikiwamo vya China, Malaysia, India, Canada, Marekani, Australia, Uingereza, Afrika Kusini na Ukraine.

Kulingana na Mollel katika maonyesho hayo wanaotaka kusoma nje wanaweza kujaza fomu hapohapo kwenye maonyesho kwa ajili ya kuanza masomo Mwaka 2017 ikiwamo mwezi Januari, Februari, Machi na kuendelea kulingana na matakwa ya mwombaji.“Wengi wamekuwa wakitaka kusoma nje, lakini baadhi wamekuwa wakishindwa kuwa na uchaguzi sahihi za nini cha kwenda kusoma, kwa hiyo kupitia maonyesho haya tutakuwa tunatoa ufafanuzi wa kozi mbalimbali,” alisema Mollel.


Waliomaliza kidato cha nne, sita na vyuo mbalimbali ni baadhi ya wale ambao wanaweza kuunganishwa na GEL kusoma vyuo vya nje ya nchi.GEL ni kampuni iliyosajiliwa Mwaka 2006 kwa lengo la kufanya shughuli za uwakala wa vyuo vya nje. Hadi sasa imeweza kuwaunganisha Watanzania zaidi ya 5400 na vyuo mbalimbali Duniani vikiwamo vya Marekani, Canada, Uingereza, Ukraine, China na India.
Mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...