Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho ya Taifa.
Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini umeikabidhi Makumbusho ya Taifa picha zilizo pigwa na wataalam wa Kijerumani kipindi cha ukoloni wa Mjerumani Tanganyika ambazo zinaonesha Majengo mbali mbali ya kihistoria hapa nchini ambayo yalijengwa kipindi cha Utawala wa kikoloni wa Ujerumani.
Akikabidhi picha hizo ambazo zilikuwa sehemu ya onesho lililofanyika kwenye makumbusho ya Kihistoria ya Berlin nchini Ujerumani, Balozi wa Ujerumani hapa nchini Mh Egon Kochanke amesema kuwa wameona kunaumuhimu mkubwa wa kuzikabidhi picha hizo Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kuonesha na kuhifadhi wa vielelezo muhimu vya kihistoria ya Tanzania.
Balozi Kochanke aliongeza kuwa hivi sasa ofisi yake inafanya jitihada za kuzunguka nchi nzima kutambua maeneo ya kihistonia ili kuona uwezekano wa namna ya kuziboresha sehemu hizo ili zibaki kama sehemu ya kumbukumbu. Hivyo ameongeza kuwa miezi michache ijayo jopo la wataalam mbali mbali kutoka Ujerumani watakuja kwa kazi hiyo.
Akipokea picha hizo za kihistoria kutoka Ubalozi wa Ujerumani, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabulla amesema kuwa picha hizi zimefika wakati muwafaka kwani zitatumika katika kuboresha onesho la kudumu la kihistoria linalotarajiwa kuboreshwa hivi karibuni.
Licha ya kumshukuru Balozi Kochanke na ujumbe wake Prof Mabulla amemuomba balozi huyo kuwa katika bajeti zao watoe kipaumbele katika masuala ya uhifadhi wa urithi wa utamaduni wa Tanzania kwani kwa sasa upo hatarini kupotea kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani na matumizi yasiyo endelevu.
Prof. Mabulla alisisitiza kuwa Ujerumani wanao wajibu mkubwa kuisaidia Tanzania kuhifadhi urithi wa utamaduni na majengo ya kihistoria ya Utawala wa kikoloni wa Ujerumani. Eneo jingine ni Makumbusho za Ujerumani kushirikiana na Makumbusho ya Taifa kuandaa na kuweka maonesho ya urithi wa Utawala wa Kikoloni wa Ujerumani hapa Tanzania, na hususani kwenye Makumbusho ya Maji Maji huko Songea.
Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabulla akipokea picha kutoka kwa Balozi wa Ujerumani Nchini Mh Egon Kochanke.
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mkuu Makumbusho ya Taifa, Balozi wa Ujetumani Nchini Mh Egon Kochanke, na afisa Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini wakiziangalia kwa umakini picha zilizokabidhiwa Makumbusho ya Taifa na Balozi huyo.
Wapili kuliani ni Mkuruganzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure akifafanua moja ya picha zilizo kabidhiwa na Balozi wa Ujerumani Nchini (wakwanza kushoto) kwenye Makumbusho hiyo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula na kulia ni Muhifadhi wa Historia Makumbusho ya Taifa Bi Flower Manase.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...