Mchezaji Riphat Hamisi wa timu ya Ndanda FC amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Novemba kwa msimu wa 2016/2017.
Riphat ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Shaban Idd wa Azam FC na Mbaraka Abeid wa Kagera Sugar.
Katika mechi mbili ambazo timu ya Ndanda FC ilicheza kwa mwezi huo, Riphat aliisaidia timu yake kupata ushindi katika michezo yote na kukusanya jumla ya pointi 6 zilizoifanya kushika nafasi ya kumi katika msimamo wa Ligi hiyo ambayo iko mapumzikoni kupisha dirisha dogo la usajili.
Pia aliifungia timu yake mabao mawili katika michezo miwili ambayo timu yake ilicheza kwa mwezi huo.
Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili zilizochezwa. Kwa kushinda tuzo hiyo, Riphat atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...