Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mshambuliaji kinda wa Azam, Farid Mussa anatarajiwa kuondoka kesho kwenda nchini Hispania kujiunga na timu yake ya Club Deportivo Tenerife baada ya safari yake kusuasua kwa muda mrefu huku ikisemekana klabu yake hiyo ikimbania kwenda kukipiga huko huku klabu yake mpya inayoshiriki ligi daraja la kwanza "segunda division" ikituma tiketi ya ndege.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Ofisa habari wa Azam, Jafari Iddy amesema kuwa safari ya Farid imeshakamilika na tayari vibali vyake vya kwenda kufanyia kazi vimeshapatikana na jana timu ya Tenerife imetuma tiketi ya ndege.
Iddy amesema kuwa, vibali vya kufanyia kazi nchini Hispania vilikuwa havijapatikana na ndiyo sababu iliyomfanya Farid achelewe kuondoka ila baada ya kupatikana tena kwa msaada mkubwa wa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.
"Tunaishukuru sana serikali kwa msaada mkubwa waliotusaidia wa kufanikisha kupatikana kwa vibali vya Farid hususani Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambaye mara nyingi alikuwa anatuulizia tumefikia wapi pamoja na ubalozi wa Hispania nchini na kwa sasa safari imekamilika kesho saa tano usiku ataondoka kuelekea nchini Hispania kwa ajili ya kuanza kazi rasmi kwenye timu yake mpya,"amesema Iddy.
Ameweka wazi kuwa Farid anakwenda nchini Hispania kwenye timu ya Tenerife kwa mkopo baada ya fedha walizotaka kuzitoa timu hiyo kuwa ni ndogo na Azam hawakuridhika nayo kwahiyo kwakuwa bado alikuwa na nia ya kucheza soka la kulipwa hawakuwa na budi ya kumuachia aende.
Ofisa habari wa klabu ya Azam Jafari Iddy akionesha tiketi ya ndege iliyotumwa na timu ya Tenerife kwa ajili ya safari ya kwenda nchini Hispania.
Mshambuliaji Farid Mussa akiwa anapambana na wachezaji wa timu ya Tenerife wakati alipokwenda kwa majaribio kwenye timu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...