Wasanii wanaowania tuzo za EATV leo walifanya semina na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kuwapa uthubutu wa kutambua vipaji vyao na kuvifanyia kazi ili kuweza kukabiliana na soko la ajira pindi watakapomaliza masomo yao.
Semina hiyo iliyoendeshwa na benki ya Barclays chini ya pango wake wa ready to Work ilifanyikakatika ukumbi wa Nyerere uliopo katika eneo la Chuo Kikuu Mlimani ambapo jumla ya wasanii 45 waliochaguliwa kuwania tunzo za EATV walihudhuria.
PICHANI JUU: Mwakilishi kutoka Barclays Bank, Joe Bendera akiongea na wanahabari waliohudhuria seminaya wasanii kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam yenye lengo la kuelimisha wanavyuo kuhusiana na kugundua vipaji vyao na kuvifanyia maamuzi baada ya masomo ilikukwepa adha ya ukwasi wa ajira inayolikabili Taifa

Lady Jaydee ambae anawania tuzo ya msanii Bora wa kike akijibu maswali ya wanafunzi
Mmoja kati ya wasanii wanaowania tunzo ya Msangi Bora wa kiume Daudi Tairo a.k.a Duma akijibu hoja za wanafunzi
Khadija Ally anayewania tuzo ya muigizaji bora wa kike akiongea wakati wa semina ya Ready to Work inayoshirikisha wasanii wanaowania tunzo za EATV
Mwakilishi wa Benki ya Barclays akijibu hoja za wanafunzi kuhusiana na mpangowa Ready to Work unaoendeshwa na benki hiyo
Mwanafunzi akiuliza swali
Mwigizaji Kajala Masanja akijibu hoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...