Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugule amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuangalia upya tozo za daladala zinazo pita katika daraja la kigamboni ili kutoa unafuu kwa wananchi waishio Kigamboni kama ilivyokuwa madhumuni ya kujengwa kwa daraja hilo.

Akizungmza na globu ya jamii Dk Ndugulile amesema kuwa wananchi wamekuwa watumwa kwa usafiri kwa miaka mingi huku wakitegemea daraja liwe mkombozi wao, lakini sasa imekuwa kinyume kutokana na gharama za kupita kwa daladala katika daraja hilo.

“gari moja yaani daladala linatakiwa kulipa shilingi 5000 kwa kila trip,jambo ambalo ni gharama kuliko biashara yenyewe ambayo ni huduma kwa wanachi hivyo kwa hesabu za haraka kama dereva atafanya trip 10 atatakiwa kulipa shilingi 50,000/- kitu hicho kinawawia vigumu kufanya kwa madereva wa daladala” amesema Dk Ndugulile.

Amesema kuwa amefanya jitihada za kila namna kwa kuzungumza na mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF ambo wao ndio wanaendesha daraja hilo kwa kuwaandikia barua rasmi  hili waweze kupunguza tozo hizo kwa ajili ya daladala lakini bado aoni dalili.

Ameongeza kuwa gharama za mkazi wa Kigamboni katika safari za mjini ni kubwa kuliko mtu yoyote licha ya kuwepo kwa miundombinu ya barabara na vivuko bado gharama za kifedha ni juu katika kutumia miundombinu hiyo.

Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugule

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...