Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Kamapuni ya Uhuru Music centre kwa kushirikiana na Dege Stationary imetoa msaada wa vifaa vya shuleni na chakula vyenye thamani ya kiasi cha fedha shilingi milioni 3 kwa ajili ya kituo cha watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Kigamboni.
Akizungumza na globu ya jamii mkurugenzi wa Uhuru Music Centre, Maneno Sanga amesema kuwa wameamua kutumia sikukuu hii kutoa zawadi kwa watoto ambao ni yatima hili nao waweze kupata maisha sawa kama watoto wengine waliopo majumbani wakiwa na wazazi wao wakati huu wa msimu wa sikukuu.
“katika zawadi hizi tumeweza kuleta vyakula ,vitabu pamoja na nguo za shule kwaajili ya watoto ambao wanataraji kujiunga na darasa la kwanza hapo mwakani hili mlezi wao asipate tabu ya kuingia gharama ya kuwanunulia vifaa” amesema Sanga.
Amesema kuwa alipowaza kutoa zawadi kwa watoto yatima alimpigia simu rafiki yake wa karibu mbunge wa Kigamboni ,Dk Faustine Ndugulile ndipo alipoweza kumuunganisha na kituo hicho cha Amani.
Kwa upande wake mbunge wa Kigamboni Dk.Faustine Ndugulile, amesema kuwa anamshukuru sana bwana Sanga kwa msaada wake kwa kushirikiana na rafiki zake kwa kuona kama Kigamboni ni sehemu muhimu ya kutoa msaada huo.
Amesema kuwa vipo vituo vingi sana na Sanga ana marafiki lakini akaona Kigamboni ndio sehemu atayopeleka zawadi hiyo kwa watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu na kuchagua kituo cha Amani kama sehemu mojawapo.
Mkurugenzi wa kituo cha Uhuru wa Music Centre, Maneno Sanga akiwa na mkurugenzi wa Dege Stationary wakikabidhi zawadi wa watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu katika kituo cha Amani.
Mtoto Melvin Ndugulile akikabidhi vitabu kwa watoto wenzie wa kituo cha Amani kilichopo kigamboni.
Mbunge wa Kigamboni ,Dk Faustine Ndugulile akibeba mzigo ambao amepeleka katika kituo hicho cha Amani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...