OFISI YA MBUNGE Jimbo La Mikumi inalaani sana kitendo cha kinyama kilichofanywa na Ndugu zetu wa jamii ya wafugaji kwa kujichukulia sheria mkononi na kumjeruhi vibaya Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi ambapo leo tarehe 25 Desemba majira ya Mchana amechomwa mkuki mdomoni na kutokezea nyuma ya shingo yake, ambapo alipelekwa hospitali ya wilayani Kilosa na baadae amekimbizwa hospitali ya mkoa Morogoro  ili kufanyiwa operesheni ya kuondoa mkuki huo na kwa matibabu zaidi.

Augustino Mtitu alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia jirani yake kufukuza Ng'ombe wasiharibu mazao shambani kwake, Kipande cha mti kinachoonekana hapo mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili kupunguza urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali,  Inasemekana MwenyeKiti wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa.
WITO KWA SERIKALI.
Ofisi Ya Mbunge Mikumi inatoa wito kwa Serikali  kuwabaini wale wote waliofanya kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria  ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA.



Imetolewa na:-
Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Mikumi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. duh hii hatari
    serikali imefeli kwenye issue ya wakilima na wafugaji
    pole saba mkulima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...