MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kutunza miti ya Korosho kwani ndio zao pekee linalowapa faida.

Ulega ameyasema hayo wilayani humo jana katika ziara yake ya kikazi katika vijiji vya Kidimni,na Msonga.ambapo aliwataka wananchi hao kutunza miti hiyo ambayo imeendelea kuwepo tangu enzi hizo.

Alisema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya utunzaji wa zao hilo Mkoa wa Mtwara,Lindi ,ikilinganishwa na Mkuranga,akaongeza kuwa Mikoa hiyo zao la Korosho wanaliheshimu mno na ndio maana hata bei zake zinachangamka.

"Nataka niwaambie mikoa ya Mtwara na Lindi ,watu wale huwezi kuwaeleza jambo lolote kuhusu Korosho kwani hata mazingira ya usafishaji wake wao wako mbele zaidi ."alisema Ulega.

Aidha katika hatua nyingine Ulega aliwataka wananchi hao kutumia fedha walizopata kutokana na uuzaji wa Korosho kukubali kutoa sh.10,000 kwa ajili ya kujiunga na Bima ya Afya ili kurahisisha upatikanaji wa matibabu.

Alisisitiza kuwa endapo watachangia fedha hizo hakutakuwa na kero ya upatikanaji wa madawa katika Zahanati zao na kama madawa hayo hayatakuwepo basi yeye kama mbunge Kazi yake ndio kusukuma Kwa wakubwa.

Licha ya hayo ulega alihaidi kutoa fedha Kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Nyumba ya mganga katika kijiji cha kidimni pamoja na mashine ya kusukuma Maji.

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Bw Abdallah Hamisi Ulega akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Kidimni katika ziara yake aliofanya jana Jimboni humo kwa lengo la Kuhimiza kuitunza na Kuheshimu zao la Korosho katika kuleta Maendeleo ya Wilaya hiyo.

Wanakijiji wa Kijiji cha Kidimni wakisikiliza kwa Makini mambo yahusuyo maendeleo ya Kijiji chao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bw Juma Abeid akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Kidimni kuhusu utunzaji wa miti ya Mikorosho katika kuleta maendeleo ya kijiji na Serikali kwa ujumla.

Picha na Yasir Adam Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...