Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amemuondoa Mpima Ardhi wa manispaa ya Musoma Mkoani Mara Bwana John Kapera na Kumtaka Katibu Tawala wa mkoa wa Mara amuondoe katika kituo chake cha kazi kuanzia kesho. 
 Bwana John Kapera amekuwa anasababisha matatizo mengi katika Manispaa hiyo na kupelekea kuwa kero kwa wananchi wa Musoma katika kupima ardhi na kumilikisha. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...