Kijana aliye patikana na hatia ni Natdanai Khongdee (Umri, Miaka 19, pichani juu wa pili kulia) ambapo mkuu wa polisi wa Nchi hiyo Chakthip Chaijinda, (wa tatu kushoto) alimtangaza mbele ya vyombo vya habari vya Nchi hiyo.
-----------------------------------------------------------------------------
Na Yusuph Kileo
Mswada wa sheria mtandao nchini Thailand uliwekwa mezani kujadiliwa takriban wiki kadhaa zilizo pita. Muswada huo ambao ulikua ukingoja kupitishwa kuwa sheria umepelekea kelele nyingi nchini humo ambapo wananchi wake walitaka ufanyiwe marekebisho kabla ya kuwa sheria huku wengine wakiukataa kabisa. 
Wana usalama mtandao nchini humo walijaribu kutoa ufafanuzi ambao haukuzaa matunda na hatimaye kutaka msaada kutoka kwa wanausalama mtandao wa maeneo mengine. 
Wiki mbili zilizo pita wahalifu mtandao Nchini humo walitangaza kushambulia tovuti za serikali  ili kushinikiza mamlaka kufanyia kazi marekebisho ya sheria hizo za mtandao ambazo walidai hawakukubaliana nazo – Baadae walianza kushambulia tovuti mbali mbali na kusababisha mtafaruku mkubwa. 
Tovuti ya polisi ya nchini humo (Royal Thai Police Office) ni miongoni mwa tovuti zilizoshambuliwa kimtandao ambapo ilidukuliwa na baadae kuangushwa kabisa. Kitu ambacho kilipelekea hasira kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo.
Naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi Mh. Prawit Wongsuwon, alitangaza kukamata washukiwa tisa (9) wa uhalifu huo mtandao pamoja  na vifaa vyao huku akiongeza  kuwa serikali ya nchi hiyo haitalinyamazia tukio hilo na kusema watachukua hatua stahiki kwa kila atakaethibitika na uhalifu huo. 
Tayari kati ya tisa (9) waliokamatwa , Kijana mdogo mmoja amepatikana na hatia huku wengine nane (8) bado wanaendelea kufanyiwa uchunguzi. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...