Watu watano wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya kudondokewa na mwamba wa mawe katika shimo la mgodi wa zamani wa Resolute, uliopo Nzega mkoani Tabora.
Akizungumzia swala hilo, Mkuu wa wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupulla alisema tukio hilo limetokea jana saa 7:00 baada ya kundi la wachimbaji wadogo wa mgodi wa Umoja kuvamia eneo hilo ambalo limepigwa marufuku na Serikali.
Alisema eneo hilo limezuiwa kuchimbwa kutokana na hatari iliyopo lakini baadhi ya wachimbaji wamekuwa wakiingia kwa kificho kuchimba.
Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Joseph Mpenda, mkazi wa shinyanga, Mohamed Mohamed mkazi wa Singida , Manona Nyombi mkazi wa Bariadi na Modesta Leonard mkazi wa Nzega.
Waliojeruhiwa ni Kangwa Mayenga mkazi wa Bariadi, Agness Antony mkazi wa Chato, Deus Alphonce mkazi wa Igunga na aliyefahamika kwa jina moja la Mapunda mkazi wa Chato. Chanzo - Mwananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...