Mh, Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg, Nape Moses Nnauye mapema Leo Asubuhi alifanya mazoezi ya pamoja na Vijana wa Lindi Fitness Club kabla ya kwenda kwenye Ziara za kuzungumza na Halmashauri kuu za kata za Jimbo la Mtama, na kupiga nao picha.

 Alitumia nafasi hiyo kuwataka Vijana kote nchini kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi ili kujenga Afya ya mwili na Akili kwa lengo la  kuepukana na magonjwa yanayosababishwa na  kutokufanya mazoezi kama vile kisukari, magonjwa ya moyo, kiharusi n.k lakini pia alisema ni kuunga mkono kauli iliyotolewa na Serikali kupitia Mh, makamu wa Rais mama Samia Suluhu kuwa kila jumamosi ya pili ya mwezi iwe ni siku ya kufanya mazoezi.

Hivyo ametoa wito kwa Vijana hususani wa jimbo la Mtama na Mkoa wa Lindi kwa ujumla wawe wa kwanza kujitokeza kila kata naye yupo tayari kuhamasisha na kusaidia upatikanaji vifaa vya michezo kupitia wadau mbalimbali wa michezo.

SABUNI H. M
Katibu wa UVCCM
Wilaya ya Lindi Vijijini.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama,Ndg, Nape Moses Nnauye mapema leo asubuhi alifanya mazoezi ya pamoja na Vijana wa Lindi Fitness Club kabla ya kwenda kwenye ziara yaa kuzungumza na Halmashauri kuu za kata za Jimbo la Mtama, na kupiga nao picha ya pamoja kama inavyoonekana pichani juu.


Mh.Nape na akiwa sambamba na Vijana wa Lindi Fitness  Club wakisikiliza maelekezo ya namna ya kufanya mazoezi katika suala zima la kujenga afya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...