Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


MABINGWA watetezi wa ligi kuu Vodacom Yanga imefanikiwa kupanda hadi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 na kuishusha Simba iliyomalizia kileleni mzunguko wa kwanza kwa pointi zake 35. 

Winga Simon Msuva aliweza kuwa nyota wa mchezo huio baada ya kufanikiwa kuifungia timu yake goli mbili katika dakika ya 57 na 90 huku lingine akipiga pande safi linalomshinda beki Michael Aidan na kuingia nao nyavuni dakika ya 38.

JKT Ruvu waliweza kucheza kandanda safi na wakionekana kutumia mashuti ya mbali kuweza kujaribu nafasi ya kufunga huku mshambuliaji wake Atupele Green akikosa nafasi mbili za wazi.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm alikuwepo jukwaa kuu kufuatilia mchezo, wakati kiungo mpya kutoka Zambia, Justin Zulu pia akiwa jukwaani kwa sababu bado hajapatiwa kibali cha kufanya kazi nchini. 

Baada ya mchezo, kocha msaidizi Juma Mwambusi amesema kuwa waliingia uwanjani na mpango wakushinda na wamefaniklisha hilo ingawa mchezo ulikuwa mgumu sana kwao.Mechi hiyo ilichezeshwa na Hery Sasii akisaidiwa na Hellen Mduma na Kassim Mpanga wote wa Dar es Salaam.

Matokeo mengine ni:
Mwadui 1-0 Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mbeya City 0-0 Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.

Kikosi cha Yanga kilikuwa; 
Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Mwinyi Hajji Mngwali, Kelvin Yondan, Vincent Bossou, Simon Msuva, Thabani Kamusoko/Geoffrey Mwashiuya dk84, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Said Juma ‘Makapu’ dk55na Deus Kaseke/Obrey Chirwa dk90
.
JKT Ruvu: Hamisi Seif, Michael Aidan, Edward Charles, Yussuf Chuma, Kelvin Nashon/Naftal Nasho dk66, Rahim Juma, Ally Bilal/Mussa Juma dk77, Hassan Dilunga, Najim Magulu, Atupele Green/Saad Kipanga dk77 na Edward Joseph.

Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Ruvu JKT  FC
Kikosi cha Ruvu JKT Ruvu leo dhidi ya  Yanga FC 
  Mchezaji wa timu ya Yanga Donald Ngoma (kati)  akiwania mpira na michezaji wa timu ya Ruvu JKT Edward Charles katika mchezo wa VPL uliomaizika kwa Yanga SC kuibuka na ushindi wa goli 3-0 leo jijini Dar es Salaam.



Mshambuliaji wa timu ya Ruvu JKT Ruvu  Naftali Nashon    akimtoka beki wa timu ya Yanga leo  katika uwanja wa Uhuru mchezo uliomaizika kwa Yanga SC kuibuka na ushindsi wa goli 3-0 leo jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa timu ya Yanga akifurahia baada ya kuifungia timu yake bao la tatu  dhidi ya Ruvu JKT  uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka, 
video na Bakari Issa Majeshi, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...