Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi amewaasa wafugaji kuacha kuingiza mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza hifadhi hizo.
Katibu Mkuu uyo aitoa wito huo wakati akizungumza baada ya kufanya matembezi ya kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff ambapo wageni mashughuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa alishiriki.
“Hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya wanyama pori pekee na siyo kwa mifugo na hivyo kila mwananchi analo jukumu la kuyalinda mazingira haya,”Aliongeza Mej.Gen Milanzi.
Awali akizungumza katibu mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina mkakati mkubwa wa kuhakikisha inashirikiana na nchi zingine katika kutokomeza kabisa Ujangili wa pembe za ndovu nchini.
Aidha aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo upigaji marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizo ifikapo mwezi machi Mwaka huu.
Rais Msataafu wa
Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa akizungumza mara baada ya
kupokea Matembezi kwa ajili ya kupinga ujangili ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 leo jijini Dar es Salaam.
Matembezi hayo ya kilomita tano yameratibiwa na Asasi ya Tanzania – China
Promotion Association (TCFPA) na Ubolozi wa China ambapo yalianzia Ofisi za
Ubalozi wa China na kuishia katika Hotel ya Sea Cliff.
Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing, akizungumza
kabla ya kuanza matembezi ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 leo
jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yana lengo la kuhamasisha
upingaji wa ujangili na mauaji ya Tembo.
Katibu Mkuu wa Asasi ya Tanzania – China
Promotion Association (TCFPA) akitoa maelekezo kuhusu matembezi ya Walk for
Elephant Dar es Salaam 2017 leo jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya
kilomita tano yameratibiwa na asasi hiyo kwa kushirikiana na Ubolozi wa China
ambapo yalianzia Ofisi za Ubalozi wa China na kuishia katika Hotel ya Sea
Cliff.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi (kushoto)
akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa matembezi
ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Lengo la matembezi hayo ni kuhamasisha jamii kupinga ujangili na mauaji ya
Tembo.
Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing, akiwaongoza
mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kufanya mazoezi kabla ya kuanza
matembezi ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 leo jijini Dar es Salaam.
Matembezi hayo ya kilomita tano yana lengo la kuhamasisha upingaji wa ujangili
na mauaji ya Tembo. Kwa habari kamili BOFYA HAPA
Chinese are so smart.........
ReplyDelete