Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)  kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kipindi cha  Julai mpaka Desemba 2016 zilifanya ukaguzi katika baadhi ya migodi mikubwa nchini na kampuni za uchimbaji madini kulipa kodi na kufanikiwa kukusanya Sh. bilioni 79.26

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari TMAA,  Mhandisi Yisambi Shiwa, amesema fedha zilizopatikana zililipwa serikalini ikiwa ni kodi ya mapato iliyotokana na ukaguzi huo. Amesema katika ukaguzi huo Kampuni ya Geita Gold Mining Limited  imelipa Sh. biliioni 45.76  pamoja na  Kampuni ya North Mara Limited imelipa  sh. bilioni 33.5

Mhandisi Yisambi amesema  ukaguzi wa madini ya ujenzi na viwandani uliofanywa na wakala kwa kushirikiana na Ofisi za Madini Kanda za Kaskazini,Mashariki,Kusini  pamoja na Magharibi umesaidia kuongezeka kwa malipo ya mrabaha serikalini kwa  kiasi cha sh. bilioni 3.8.
‘’Kiasi cha mrabaha huo kimetokana na uzalishaji wa tani milioni 6.8 za madini ya ujenzi na viwandani yenye  thamani ya shilingi bilioni 119.5’’amesema Shiwa.

 Aidha amesema kupitia madawati ya ukaguzi yaliyopo katika Viwanja vya Ndege Nchini Wakala kwa kushirikiana na taasisi za serikali wamekuwa wakiwakamata watu wanaosafarisha madini nje ya nchi kinyume cha sheria walipigwa faini ya  Dola za Kimarekani 91,924.38 katika kipindi cha Julai na Desemba 2016.

‘’Wahusika  waliohusika na sakata la usafirishaji wa madini nje ya nchi walichukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha habari TMAA, Mhandisi Yisambi Shiwa Akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu shughuli mbalilmbali zinazowafanywa na wakala wa ukaguzi wa madini leo jijini Dar es Salaam. Kulia Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya Madini , Migodi ya Kati na Midogo, Mhandisi George Manyama. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...