Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba  Serikali zote Mbili Tanzania ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea  kujenga mazingira ya kuwapatia makaazi bora wafanyakazi wa Umma ili kuwapunguzia ukali za maisha wanayokabiliana nao kila siku.

Alisema Serikali hizo zinatambua  wazi kuwa watumishi wa Umma wanapopatiwa makaazi bora ya kuishi hata utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo ya kazi unaimarika  mara dufu.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika hafla ya ufunguzi wa Nyumba za kuishi Maafisa na Askari wa Uhamiaji hapo Mtaa wa Ndugukitu Chake Chake Kisiwani Pemba ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Alisema  ujenzi wa nyumba za watumishi nchini unatiliwa mkazo hasa wale wa Idara  ya Uhamiaji ambao ni macho ya Taifa kwa vile muda wao wote wamekuwa wakiutumia kusimamia usalama wa Taifa kwa kuwatambua  na kuwagundua wageni wote wanaoingia Nchini kinyumecha Sheria  na utaratibu zilizowekwa.

Balozi Seif  alisema Makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa hapo nyuma kati ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar  kuhusu kufunguliwa kwa Ofisi ndogo za SMT Visiwani Zanzibar ni vyema yakatekelezwa haraka iwezekanavyo hasa kwa zile Taasisi za Muungano ambazo hadi wakati huu hazijaitumia fursa hiyo.

Akizungumzia hali ya Amani na Usalama  iliyopo Nchini inayowapa Fursa Wananchi kufanya shughuli zao kama kawaida Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliliagiza Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji Tanzania kuendelea kusimamia vyema hali hiyo.

Balozi Seif alisema  wapo baadhi ya Watu hasa wale wenye asili ya Tanzania ambao tayari wameshaukataa na kubadilisha Uraia wao wamekuwa na tabia mbovu zinazowashawishi pia kujihusisha na masuala ya Kisiasa jambo ambalo wanaelewa vyema kuwa wanavunja sheria na Taratibu za Nchi.
Akitoa Salamu katika hafla hiyo fupi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Tanzania Meja General Projestus Rwegasira  alisema Idara ya Uhamiaji imekuwa na  Mkakati wa muda mrefu katika azma yake ya kuimarisha mazingira bora ya Jeshi hillo.

Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Mambo ya Ndani alisisitiza kwamba lengo la Idara ya Uhamiaji pamoja na masuala mengine iliyopangiwa kutekeleza, lakini pia imekusudia kujenga Ofisi sambamba na Nyumba za Kuishi Watendaji wa Jeshi hilo katika Wilaya zote Nchini Tanzania.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/1/2017.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilikagua Jengo la Gorofa Mbili litakalobeba Familia Sita za Maafisa na Askari wa Uhamiaji  baada ya kulizindua rasmi hapo Mtaa wa Mtukitu  Chake  chake Kisiwani  Pemba ikiwa ni sherehe za kutimia Miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi, Maafisa wa Uhamiaji na Wizara ya Mambo ya Ndani walioshuhudia ufunguzi wa Jengo la Makaazi ya Maafisa na Askari wa Uhamiaji chake chake Pemba.Kuluia ya Balozi Seif ni Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Johari Msoud Sururu,Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Meja Gneral Projestus Rwegasira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh., Mohamed Aboud Mohamed. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Mwnajuma Majid,Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiam Iddi na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga.
 Muonekano wa Haiba ya Jengo Jipya la Makaazi ya  Maafisa na Askari wa Uhamiaji liliopo katika Mtaa wa Mtukitu Chake Chake Kisiwani Pemba.
 Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu akitoa Taarifa ya ujenzi wa jengo la Makaazi ya Maafisa na Askari wa Uhamiaji wakati wa hafla ya kulizindua rasmi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Meja General Projestus Rwegasira akitoa salamu katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Makaazi ya Askari wa Uhamiaji Chake chake Pemba.

ndi cha Utamaduni cha Mkuta Ngoma cha Mkoa wa Kusini Pemba kikitumbuiza kwenye hafla ya ufunguzi wa Jengo la Makaazi ya Maafisa na Askari wa Uhamiaji Chake Chakle Pemba. Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...