WAKAZI wa jiji la DAR ES SALAAM wamepongeza huduma mbali mbali za matibabu zinazotolewa kwenye Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo kwenye hospitali ya TAIFA ya MUHIMBILI,ambapo wamesema kuwa kwa sasa matibabu ya moyo yamepata ufumbuzi tofauti na miaka mingine ilivyokuwa hapa nchini.
Wakizungumza hospitalini hapo, baadhi ya wananchi hao waliokuwa katika nyuso za furaha mara baada ya kupata huduma nzuri, wameeleza kuwa hospitali hiyo inafaa kuwa mfano wa kuigwa kutokana na namna ya huduma zinavtolewa kuanzia madaktari mpaka wauguzi na watoa huduma wa kawaida.
REUBEN MTAITA (79) mkazi wa KONGOWE nje kidogo ya jiji la DAR ES SALAAM amesema tangu ameanza kutibiwa katika hospitali hiyo ameweza kupata nafuu kwa matatizo ya moyo yanayomsumbua, huku akibainisha kuwa huduma ziko katika viwango na hujutii kupata matibabu katika hospitali hiyo.
“Ni kweli na wazi hospitali hii inatoa huduma bora kabisa , hata namna madaktari wanavyokuhudumia inatia moyo, na kwamba wako karibu na wagonjwa kuhakikisha unapata matibabu sahihi”alisema MTAITA
Kwa upande wake mkazi wa TEMEKE KHADIJA OMARY(30) amesema anafuraha huduma za hospitali hiyo na kwamba tangu aanze kutibiwa ameona unafuu mkubwa na kwamba hali yake inazidi kuimirika.
“Huduma zipo kwenye ubora na wagonjwa tuna hudumiwa bila ubaguzi hili jambo limenifurahisha kabisa”alisema KHADIJA.
Baadhi ya madaktari, BASHIR NYANGASA na GEORGE LONGOPA wamesema kwamba wanajitahidi kwa uwezo wao kuhakiksha wagonjwa wanapata matibabu ya uhakika na yenye viwango vya juu ili kuhakikisha wagonjwa wa moyo wanakuwa salama .
“Tunajitahidi kwa uwezo wetu kuwahudumia wagonjwa wote wanaofika katika taasisi yetu katika kiwango cha hali ya juu na kama ulivyoona mwenyewe, wagonjwa wanaridhika na matibabu wanayopata” alisema Dkt.NYANGASA alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa habari hii
Naye mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya MOYO YA JAKAYA KIKWETE Professa Mohamed Janabi, amesema kwamba ,katika hospitali hiyo wanaendelea kutoa huduma zilizo bora na kuwashauri wananchi nchini kujiuga na huduma za bima afya ili kuweza kumudu gharama za ugonjwa wa moyo katika matibabu na vipimo vyake.
“Mwananchi akiwa kwenye mpango wa bima ya afya ni rahisi sana ana unafuu katika kutibwa kwani ni gharama kubwa , lakini mtu anapokuwa amejiunga katika mfuko wa bima ya taifa unaweza kugharimia “ alisema Dkt.Janabi.
Amesema kwa sasa hospitai hiyo iamdelea na maboresho mbali mbali hasa katikaeneo la huduma kwa wateja ambapo amesema wafanyakazi waliopo katika idara hiyo wanapataiwa mafunzo mbali mbali ya kuweza kuhudumia wagnjwa wanaokuja katuka taasisi hhiyo.
Kwa mujibu wa Dkt.Janabi mpaka sasa taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015 mwaka jana iliweza kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa wenye jumla ya 973 ambapo ameongeza kuwa hospitali hiyo imepunguza kwa asilimia 80 kwa wagonjwa kwenda nje ya nchi kutibiwa na badala yake hutibiwa hapa nchini katka hospitali hiyo kutokana na wataalamu waliopo .
Hata hivyo amesema mbali na wagonjwa wa hapa nchin kutibiwa katika hosptali hiyo pia wagonjwa kutoka nchini za Comoro,Burundi,Congo na Uganda wamekuwa wakitibiwa katika taasisi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...