Benki
ya Exim Tanzania hivi karibuni ilitunukiwa tuzo mbili katika hafla
iliyoandaliwa na Shirikisho la Waajiri Tanzania (ATE). Benki ya Exim ilishinda
tuzo ya Uongozi na Utawala- Rasilimali Watu (HR- Leadership & Governance)
na tuzo ya Ushirikisho wa Wafanyakazi (Employee engagement). Tuzo hizo mbili
muhimu zilitolewa kwa benki katika hafla ya mfanyakazi bora wa mwaka 2016 na
zilikabidhiwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi.
Utawala
bora katika kitengo cha rasilimali watu na ushirikishwaji wa wafanyakazi ni
nguzo muhimu katika uendeshaji wa kitengo hicho cha Exim ambacho hufanya kazi
ya kuhakikisha wafanyakazi wanatekeleza majukumu yao katika namna ambayo inayohakikisha
benki inafanikisha mipango na malengo yake huku ikiendelea kupata faida kila
mwaka. Mwaka 2016 Exim ilitimiza miaka 19 ya operesheni huku ikifanya bidii
katika kuongeza viwango vya kushirikisha wafanyakazi wake katika shirika hilo.
Benki
ilifanya vizuri sana katika kuhamasisha utawala bora na ushirikishwaji
wafanyakazi kupitia njia nyingi za asili. Benki ilipitia upya sera ya
rasilimali watu na kuongeza vifungu vinavyohamasisha wafanyakazi kuwa na maisha
yenye afya bora. Benki iliingia katika mchakato wa kuimarisha mfumo wa kufanya
tathmini ya utendaji ambao ni wa kisasa na umeunganishwa katika mfumo ulioko
mtandaoni unaoitwa Adrenalin ambao ni wa uwazi sana.
Katika
uajiri mkakati mkuu ulikuwa ni kuhakikisha usawa wa jinsia katika wafanyakazi wa kike na kume
ambao jumla yao wanafikia 1000. Benki inahakikisha kuwa wafanyakazi watendaji bora
wanatambuliwa kupitia tuzo za wafanyakazi, tuzo za wafanyakazi wa muda mrefu,
kupandishwa vyeo kutoka nafasi za chini kwenda kwenye nafasi za kati hadi nafasi
za juu za umeneja katika shirika kupitia matangazo ya nafasi za kazi ya ndani
na programu ya uwezo inayoitwa HIPO. Benki pia iliboresha miundo ya vitengo
vyake vyote, kuboresha vyeo na kufanya tathmini za ajira ambazo ziliboresha
mifumo ya kazi na hivyo kusababisha usimamizi mzuri na uzalishaji katika
vitengo. Vilevile benki iliboresha mifumo ya mawasiliano kupitia majukwaa ya
majadiliaano kati ya menejimenti na wafanyakazi ili kujadili utendaji wa benki
na kupeana mrejesho uliolenga kuimarisha utendaji wa benki.
Kwa
upange mwingine benki ya Exim imekuwa ikitumia teknolojia ili kuwapatia
wafanyakazi zana bora za kuongeza uzalishaji, kuboresha huduma kwa wateja na
mafunzo na maendeleo. Benki ilijikita katika miradi kadhaa iliyolenga
kutekeleza teknolojia mbalimbali katika utendaji kwa kuweka namba maalum “whistleblower” inayoweza kutumika na wafanyakazi na wateja pia kutoa
taarifa za kiutendaji za benki ikiweka benki katika jukwaa la kidijitali zaidi.
Katika
mafunzo na maendeleo, benki ilianzisha mfumo wa
kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika. Kusudi la Elimika ni kutoa
maarifa kwa wafanyakazi kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika katika utendaji wa
kazi zao. Matokeo ya Elimika ni wafanyakazi walioelimika zaidi, wenye uelewa na
ushirika zaidi. Kasi ya mageuzi haya imekuwa kubwa na kuleta ukuaji katika
biashara nchini Tanzania na kuwezesha wafanyakazi walio makao makuu kuweza
kutoa msaada na ushirikiano kwa wengine mikoani na katika kampuni tanzu.
“Exim inajivunia
kuwa benki ambayo inajikita katika uvumbuzi na teknolojia. Tunatumia suluhisho
za teknolojia ili kutengeneza mazingira yanayoboresha kwa kiwango kikubwa uwezo
wa wafanyakazi. Kozi hizi zinasaidia wafanyakazi kuwa na uelewa mkubwa wa
majukumu yao na pia kuwa na zana za vitendo kuendeleza ujuzi na vipaji vyao,”
alisema Fredrick Kanga ambaye ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu cha Exim.
“Ni matumaini
yetu kuwa wafanyakazi wetu wataendelea kujenga ujuzi wao kupitia Elimika. Na
menejimenti ya Exim itaendelea kuboresha mifumo yake ili tuendelee kuwa
mwaajiri bora kabisa nchini. Nina imani kubwa kuwa tuna uwezo huo na tumeamua
kuileta Exim katika kiwango hicho mwaka huu,” alimalizia Fredrick Kanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...