Kiungo wa Hull City Ryan Mason amefanyiwa upasuaji baada ya kuumia fuvu la kichwa kwenye mchezo dhidi ya chelsea hapo jana.

Mason aligongana na Gary Cahill wakati wakiwania mpira mnamo dakika ya 13 na kutolewa nje huku akisaidiwa na mashine ya kupumulia na kupatiwa huduma ya kwanza kwa muda wa dakika 8 kisha kukimbizwa hospitalini.

Taarifa toka ndani ya klabu yake ya Hull City zimedai kuwa Mason yupo katika hali nzuri na anategemewa kusalia hospitalini kwa siku kadhaa pamoja na kuwashukuru watoa huduma ya kwanza pamoja na wauguzi wote waliomsaidia mchezaji wao.

Upande wa Gary Cahill amemtakia Masona afya njema mapema sawa na wachezaji wengine wengi pamoja na kocha wa Chelsea Antonio Conte

 Kocha mkuu wa Chelsea Antonio Conte alisema: "Kila mtu katika klabu ya Chelsea wanampa pole Ryan Masom kwa matatizo aliyoyapata kwani ilikuwa ni ajali mbaya katui yake na Gary Cahill.



      Kila mtu katika timu yetu ya  Chelsea, tunatarajia kumuona Mason akirejea  uwanjani na kupona haraka sana.



Matukiuo ya uwanjani baada ya kuumia kwa Ray Mason jana katika mchezo wa Hully City na Chelsea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...